Tuesday, 22 September 2015

JUA FAIDA ZA MATUNDA MBALI MBALI

 


                                      FAIDA ZA JUISI YA UKWAJU.

  1. Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
  2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
  3. Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
  4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
  5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
  6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
  7. Husaidia kurahisisha choo (laxative)
  8. Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
  9. Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
  10. Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)

                   MAPARACHICHI  PEA (AVOCADO)

       Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana ukilinganisha na matunda mengine lakini kuna mafuta mengi na unaweza kuchanganya kula na tunda lingine kama vile apple, ndizi, chungwa au hata maziwa kwa kutengeneza juisi.

                                           TINDIKALI
Licha ya kuwa na mafuta parachichi lina tindikali (acid) mbalimbali ikiwemo inayojulikana kama amino ambayo husaidia sana kukinga na kutibu maradhi katika mwili wa binadamu. Tunda hili pia lina protini ya kiwango cha juu.

Pia kuna tindikali inayoitwa oleic acid kwenye parachichi ambayo husaidia kukinga magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa.


                                        VITAMINI “E” NA B6
Imeelezwa na wataalamu kuwa tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini E kuliko ile inayopatikana kutoka kwenye mazao ya wanyama.Parachichi lina vitamini hiyo nyingi kuliko inayopatikana katika mayai ambayo yanasifika kwa kuwa na vitamini e, hivyo hii inathibitisha kuwa lina faida kubwa mwilini.

Licha ya vitamini E pia ndani ya parachichi kuna vitamini B6 na kuna madini ya chuma (Iron) kwa wingi na madini ya potassium, pamoja na vitamin B6 na E mlaji anaweza kuletawa nafuu sana kama alikuwa na matatizo ya stress, matatizo ya uzazi kama ugumba na jogoo kutopanda mtungi Nguvu za kiume pia tunda hili linasaidia (impotence) .


                                   FAIDA ZA PARACHICHI
Licha ya binadamu kufaidika na virutubisho vya tunda hili kuna faida nyingi za parachichi kama vile majani ya mti wake pamoja na magamba, baadhi ya watu hutumia kutibu maradhi ya kuharisha.

Majani na magamba hayo hutibu pia tatizo la gesi tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa dawa za mitishamba, dawa hii haifai kutumiwa na wanawake ambao wana mimba kwani wakitumia inaweza kusababisha kuharibika kwa ujauzito.

HEDHI
Hata hivyo, wataalamu wa tiba mbadala wanasema dawa hiyo inaweza kuwasaidia sana wanawake ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati, na wakitumia vyema wanaweza kuanza kuona siku zao.

Aidha, tunda hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani parachichi lina nyuzinyuzi “fiber” ambayo ni muhimu kukinga kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya mishipa ya moyo hasa wa artery wanashauriwa kula tunda hili mara nyingi.

Lakini pia tunda hili limethibitishwa na wataalamu kuwa linapunguza kwa kiwango kikubwa cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa watu wanene.

Tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa mikunjo, hung`arisha na kulainisha nywele na kuzisaidia kukua pia kuziimarisha na kuzuia kukatikakatika.

Parachichi unaweza kulila kwa kulimenya au kwa kulisaga na kutengeneza juisi na kama nilivyoeleza hapo juu unaweza kuchanganya na matunda mengine kama tulivyoyataja na hutaharibu virutubisho vilivyomo badala yake utaongeza ubora wa juisi yako.

Watoto wadogo pia unaweza kuwapa tunda hili na wakafaidika na haya tuliyoyaandika.
Parachichi pia huweza kutumika kama siagi kwa kupaka kwenye mkate au kuchanganya na wali.

Haya wale wanaopenda ngozi zao za mwilini zisijikunje hata wakiwa watu wazima wadumu kula tunda hili kila siku katika maisha yao basi ngozi za mwili wao hazitajikunja hata usoni watakuwa kila siku vijana hata wakiwa wazee.

 

                                           PAPAI

 Watu wengi hulitumia tunda la papai kwa sababu ya utamu wake.
Hata hivyo mbali na kuwa na ladha nzuri, tunda la papai lina faida lukuki kwa afya ya mwanadamu.

UTAJIRI WA VITAMINI
Tunda la papai lina vitamini A,B,C,D, na E jambo linalo liweka tunda hili katika kundi la matunda na vyakula vyenye utajiri mkubwa wa vitamin.
Mti wa papai
FAIDA ZA KIAFYA ZA TUNDA LA PAPAI
Tunda la papai lina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa :
Mbegu za Papai
1. Kutibu tatizo la Shida ya kusaga chakula tumboni
2. Kutibu Udhaifu wa tumbo
3. Kutibu Kisukari na asthma au pumu.
4. Kutibu Kikohozi kitokacho mapafuni
Mizizi Ya Papai
5. Kutibu Kifua kikuu
6. Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku
7. Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda
8. Vilevile yanasaidia kutibu sehemu palipoungua moto
9. Kama hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na Ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani)
Majani Ya Mpapai
10. Pia yanasaidia kutofunga choo
11. Maganda ya tunda la papai yanasaidia kutibu tatizo la kuungua, vipele na saratani ya ngozi.
12. Mbegu zake zinatibu ini zikitafunwa 10 – 12 kwa siku 5.
13. Majani yake yakaushie ndani, yanatibu pumu. Inapoanza kubana yachome majani yaliyokaushwa kisha jifukize, kule kubanwa kutakisha.
14. Majani yake yanasaidia katika kutibu shinikizo la damu.
15. Papai likimenywa na kupondwa linafaa Sana katika masuala ya urembo kwani linaweza kutumika Kama vile unavyotumia lotion kulainisha uso.
16. Mbegu za papai zina uwezo wa kutibu homa. Meza mbegu za papai kiasi cha kijiko cha chakula mara 3 kwa ajili ya kutibu homa.
17. Mbegu za papai zilizokaushwa ndani kisha zikasagwa kuwa unga zinatibu malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji, kunywa mara 3 kwa siku 5 Mgonjwa wa kifua kikuu akila matunda haya kwa muda mrefu atapona bila dawa nyingine.
18. Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita 2 na nusu kwa dakika 15, yanatibu figo, bladder, yanazuia kutapika. Nusu kikombe cha chai kutwa mara 3 kwa siku 5.
 

                                                FAIDA ZA  NANASI 

   UTAJIRI  WA  VITAMINI  NA  MADINI :

Nanasi ina vitamini A,B na C na pia ina madini ya chuma, calcium, copper na phosphorous ambayo  yote  ni  muhimu  sana  katika  afya  ya  mwanadamu.
ii.           Tunda hili husaidia kutengeneza damu
iii.         Nanasi  husaidia  kuimarisha mifupa , meno, neva na misuli (muscles).
iv.         Tunda  la  nanasi  hutibu matatizo ya tumbo.
v.           Hutibu  matatizo  ya  Bandama
vi.         Hutibu  matatizo  ya   Ini
vii.       Husaidia  kusafisha   Utumbo mwembamba
viii.     Husaidia  kutibu  Homa
ix.         Husaidia  kutibu Vidonda mdomoni
x.           Husaidia  kutibu   Magonjwa ya koo
xi.         Husaidia  kutibu  tatizo  la  Kupoteza kumbukumbu
xii.       Husaidia  kutibu  maradhi ya akili Kukosa mori (low spirit)
xiii.     Husaidia  kutibu  Kikohozi
xiv.     Husaidia  kutibu  tatizo  la Kutetemeka
xv.       Husaidia  kutibu  tatizo  la Woga ( Anxiety )
xvi.     Husaidia kutibu  matatizo ya wanawake (upungufu wa hormones au makosa fulani katika sehemu za siri )
xvii.   Huondoa shida ya kufunga choo
xviii. Hutibu  tatizo  la  baridi yabisi
xix.     Husaidia  katika  kutibu  tatizo  la  Upungufu wa damu
xx.       Pia  tunda  hili   huwasaidia  akina mama wanaonyonyesha (wenye maziwa machache)

No comments:

Post a Comment