Saturday, 26 September 2015

UTENGEZAJI WA JUIS MBALIMBALI


                                                  JUISI YA UKWAJU

Tokeo la picha la ukwajuHuhitaji kutumia gharama kubwa na ni rahisi kutengeneza juisi hii ya ukwaju.
Mahitaji:
-Maji ya moto lita moja
-Ukwaju wa kutosha
-Jagi au birika lenye uwezo wa kutosha maji lita moja au zaidi

Jinsi ya kutengeneza:
Weka maji yako ya moto kwenye jagi au birika lako kisha weka ukwaju ndani yake (ukwaju uliotolewa maganda). Acha ukwaju ndani ya maji ya moto kwa muda hadi maji yatakapopoa kabisa. Baada ya hapo koroga mchanganyiko huo hadi uhakikishe kuwa juisi imekuwa nzito.
Kisha mimina juisi yako kwenye jagi lingine kuchuja mabaki ya ukwaju (usichuje juisi kwa chujio la chai). Baada ya hapo juisi yako itakuwa tayari kutumika. Lakini usiweke sukari wala kitu kingine chochote kwenye juisi hiyo. Sasa unaweza kuanza kunywa juisi yako. Sio lazima uimalize yote kwa mkupuo, lakini hakikisha kuwa unaimaliza ndani ya dakika kama kumi hadi kumi na tano.

Baada ya kuimaliza juisi hiyo na kukaa kwa muda wa kama nusu saa au zaidi utaanza kuona mabadiliko kwenye tumbo lako. Tumbo litavurugika na utaanza kuharisha mara kwa mara. Hilo sikuogopeshe wala kukupa wasiwasi, kwani hapo ndio dawa inafanya kazi ya kusafisha. Lakini ukiona kuwa baada ya kunywa juisi hiyo na muda unazidi kwenda, nusu saa, mara saa moja na kuendelea lakini tumbo halivurugiki na hupati hamu ya kwenda chooni ujue dawa haijakolea. Utakachotakiwa ni kutengeneza juisi nyingine siku nyingine lakini mara hii weka maji zaidi ya lita moja na ukwaju mwingi zaidi.

Matokeo ya dawa hii huanza kuonekana baada ya wiki mbili na kuendelea.

Jitahidi kama utaweza jiwekee utaratibu wa kunywa juisi ya aina hii angalau mara moja kila mwezi kwani haina gharama na haina madhara mwilini.

Kumbuka pia yafutayo ni muhimu;
-Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara
-Kunywa maji mengi
-Kula mlo wenye mpangilio mzuri

       
                                                     JUISI YA TENDE

 Tokeo la picha la PICHA tende
 Mahitaji 
Maziwa - Tende  -  Karanga unaweza pia kutumia almonds(lozi),korosho

Namna ya kutengeza.

Toa tende makokwa

Weka katika blender pamoja na maziwa au aina ya nuts upendayo

Saga hadi iwe laini iwe kama uji mzito kiasi

Weka kwa friji ipate baridi kidogo

Then enjoy juice ya tende......


                                     JUISI MJANGANYIKO
FAIDA YA JUICE YA MATUNDA MCHANGANYIKO KAMA TIBA YA MWILI WA BINADAMU.
Katika ulimwengu wa vyakula,inafahamika na kuaminika kuwa chakula ni dawa. Chakula unachokula leo ndicho kinachoamua hali yako ya kiafya kesho. Unaweza kuishi bila kuugua kama ukila vyakula vyote muhimu vinavyohitajika mwilini.
Leo nitakutajia orodha ya juice zilizotengenezwa kwa matunda na mboga na faida zake mwilini. Katika orodha hii, utaona kuna mchanganyiko wa matunda au mboga mbili hadi nne na kazi zake mwilini, zikitumika kama tiba au kinga ya magojwa.
KAROTI,TANGAWIZI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda hayo matatu huondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili.Tufaa ndiyo apple kwa kiingereza.
TUFAA,TANGO NA FIGILI
Juice ye ye mchanganyiko wa matunda haya ni kinga dhidi ya saratani,huondoa lehemu (cholestrol) mwilini,husafisha tumbo na pia huondoa maumivu ya kichwa.
NYANYA,KAROTI NA TUFAHA
Juice yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya ngozi ya mwili kuwa nyororo na huondoa harufu mbaya mdomoni.
TUFAA NA TANGO
Juice yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili.
CHUNGWA,TANGAWIZI NA TANGO
Juice yenye mchanganyiko wa matunda haya hung'arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini,pia hupunguza joto la mwili.Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juice hii itawasaidia sana.
NANASI,TUFAHA NA TIKITIMAJI
Juice yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini,husafisha kibofu cha mkojo na figo. juice hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu au au wanaotaka kujikinga na magojwa hayo.
TUFAA,TANGO NA 'KIWI'
Juice yenye mchanganyiko wa matunda haya hung'arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni aina ya matunda ambayo hujulikana pia kama 'matunda damu'.
PEASI NA NDIZI
Juice yenye mchanganyiko wa matunda haya hurekebisha kiwango cha sukari katika damu.Inawafaa sana wagojwa wa kisukari na inaweza kuwa sawa na kinga dhidi ya ugojwa huo.
KAROTI,PEASI TUFAHA NA EMBE
Juice yenye mchanganyiko wa matunda haya huzuia athari ya sumu mwilini, hupunguza shinikizo la damu na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.
MASEGA YA ASALI,ZABIBU,TIKITIMAJI NA MAZIWA
Juice yenye mchanganyiko huu huwa na kiasi kikubwa cha Vitamin C na Vitamin B2 ambazo huimarisha chembechembe hai na kinga ya mwili.
PAPAI,NANASI NA MAZIWA
Juice hii inakiwango kikubwa cha Vitamin C,E na madini ya chuma. Huimarisha rangi ya ngozi na mfumo wa usagaji chakula tumboni.
NDIZI,NANASI NA MAZIWA
Juice hii yenye kiasi kikubwa cha Vitamin na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini,huzuia tatizo la ukosefu wa choo.
ILI KUPATA FAIDA ZILIZOAINISHWA KATIKAKUNDI LA MATUNDA HAYO,USAFI WA MATUNDAYENYEWE HAUNA BUDI KUZINGATIWA EAKATI WA KUTAYARISHA JUICE YAKE. VILEVILE HAKIKISHA UNATUMIA MATUNDA YALIYOIVA VIZURI NA UYATAYARISHE VIZURI KWA KUZINGATIA KANUNI ZA USAFI 'MTU NI AFYA'
UNAWEZA KUTUMIA MASHINE MAALUM YA KUKAMULIA MATUNDA (BLENDER) AU KUTUMIA NJIA YA ASILI YA KUTWANGA KWA KINU MAALUMU NA KUPATA JUICE HIYO. KAMA UTAONGEZA SUKARI INASHAURIWA KUWEKA KIASI KIDOGO SANA. NI BORA ZAIDI USIPOWEKA SUKARI,KWA SABABU MATUNDA MENGI YANA SUKARI YA ASILI.

6 comments: